Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) – ABNA – Kundi la Wanafunzi wa kike kutoka Chuo Kikuu cha Gilan walitembelea Makao Makuu ya Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) na kukutana na Ayatollah Reza Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo na Mwakilishi wa Wananchi wa Mkoa wa Gilan katika Bunge la Wataalamu wa Uongozi.
1 Mei 2025 - 18:30
News ID: 1554062
Katika ziara hiyo, Wanafunzi hao wa Chuo Kikuu waliweza kufanya mazungumzo ya kina na Ayatollah Ramezani, sambamba na kujadiliana juu ya namna sahihi na nzuri ya kuongeza uelewa wa Wanafunzi kuhusu nafasi ya Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake (a.s) katika Uislamu, na umuhimu wa kujipamba kwa maadili mazuri ya Kiislamu katika jamii ya kisasa.
Your Comment