Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - Abna - Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa "Wanahabari wa Ahlul-Bayt (a.s)" umefanyika leo asubuhi kwa mnasaba wa maadhimisho ya "Dahe Karamat / (Siku Kumi za Karamat) / The Ten Days of Karamat" kwa ushiriki wa Wanahabari na Wasomi kutoka Iran na Bara la Afrika. Tukio hili limeandaliwa na Shirika la Habari la Abna na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) Mjini Qom.

1 Mei 2025 - 18:53

Ripoti ya Picha | Matukio ya Kando ya Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Wanahabari wa Ahlul-Bayt (a.s) kwa Ushiriki wa Wanahabari kutoka Bara la Afrika

Mkutano huo wa Kimataifa ulilenga kuimarisha ushirikiano wa Vyombo vya Habari vya Kiislamu, hasa katika kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s) na kukabiliana na kampeni za upotoshaji kuhusu Uislamu zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Magharibi.

Washiriki walijadiliana kuhusu changamoto zinazoikabili jamii ya Kiislamu katika uga wa habari, umuhimu wa kutumia teknolojia ya kisasa ikiwemo akili bandia (Artificial Intelligence), na umuhimu wa kuwasilisha Uislamu wa kweli na halisi unaojengwa juu ya misingi ya haki, huruma, uadlifu, na heshima ya Mwanadamu.

Aidha, tukio hilo liliambatana na maonyesho ya kazi za vyombo vya habari vinavyohusiana na Ahlul-Bayt (a.s), pamoja na uzinduzi wa miradi mipya ya usambazaji wa habari kwa lugha mbalimbali za Bara la Afrika.

Your Comment

You are replying to: .
captcha