Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Sherehe ya kuwatunuku Walimu bora – Wanawake na Wanaume – imefanyika nchini Burundi kwa lengo la kuadhimisha Siku ya Mwalimu Duniani. Tukio hili lililenga kutambua mchango mkubwa wa walimu katika elimu na maendeleo ya jamii. Walimu walioteuliwa walipokea vyeti na zawadi kama ishara ya shukrani kwa kazi yao ya kujitolea na ufanisi kazini. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu, wakiwemo viongozi wa serikali, walimu, wazazi na wanafunzi, na ilitawaliwa na hotuba za kuhamasisha juhudi zaidi katika sekta ya elimu.
Miongoni mwa walimu waliotunukiwa ni Sheikh Khamis Sadiq, ambaye alipokea tuzo ya heshima kwa kujitolea kwake katika kufundisha na kulea wanafunzi kwa weledi na maadili mema. Hafla hiyo ililenga sio tu kutoa zawadi na vyeti kwa walimu bora, bali pia kuhamasisha jamii kuendelea kuthamini nafasi ya walimu kama nguzo kuu ya maendeleo ya taifa.
Mgeni rasmi alipongeza juhudi za walimu katika kulea kizazi chenye maarifa na maadili
Tizama picha zaidi za tukio hili tulizokuwekea hapo chini
Your Comment