Programu hii, inayofanyika kila siku asubuhi kabla ya masomo, imepokelewa kwa hamasa kubwa na inasimamiwa na walimu wenye uzoefu wa Elimu ya Tajwidi na Maarifa ya Qur'an Tukufu.

5 Mei 2025 - 18:10

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Leo, Tarehe: 5 Mei, 2025, Shule ya Imam al-Hadi (a.s) iliyoko nchini Malawi, chini ya Usimamizi wa Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s), Hojjat Al-Islam wal-Muslimin, Dr. Ali Taqavi, imeendelea na programu yake ya kila siku ya Usomaji wa Qur’an Tukufu, inayolenga kuwalea Wanafunzi katika mazingira ya kiroho, nidhamu na upendo kwa Kitabu hiki Kitukufu.

Programu hii, inayofanyika kila siku asubuhi kabla ya masomo, imepokelewa kwa hamasa kubwa na inasimamiwa na walimu wenye uzoefu wa Elimu ya Tajwidi na Maarifa ya Qur'an Tukufu. Wanafunzi hawa huchukua nafasi kwa zamu kusoma Qur’an Tukufu kwa lafudhi sahihi na kupitia Maqamat mbalimbali ya kitaalamu, huku wakihimizwa kuelewa maana na ujumbe wa Aya wanazozisoma.

Lengo kuu ni kuimarisha maadili, nidhamu, na kumjenga Mwanafunzi katika msingi imara wa Kiislamu tangu utotoni.

Programu ya Kila Siku ya Usomaji wa Qur’an Tukufu katika Hawza ya Imam al-Hadi (a.s), Malawi + Picha

#UsomajiWaQuran #ShuleYaKiislamu #ImamAlHadi_Nchini_Malawi #ElimuNaMaadili

Your Comment

You are replying to: .
captcha