Ziara hii ni muendelezo wa juhudi za kuimarisha mawasiliano kati ya Madhehebu mbalimbali za Kiislamu na kujenga jukwaa la pamoja la kuhudumia jamii ya Kiislamu nchini Tanzania.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Leo [Tarehe 07 - 05 - 2025], Dkt. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Jamiat Al-Mustafa (s.a.w.w) nchini Tanzania, Dar-es-Salam, amefanya ziara rasmi ya siku moja katika Mkoa wa Tanga- Tanzania. Katika ziara hiyo muhimu, Dkt. Ali Taqavi alikutana na kufanya kikao cha mazungumzo na viongozi wa kidini kutoka Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) wa Mkoa huo.
Akiongozana na Samahat Sheikh Dkt. Al-Had Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), ujumbe huo ulilenga kuendeleza mashauriano na kukuza maelewano baina ya madhehebu ya Kiislamu nchini Tanzania. Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa mshikamano wa Waislamu licha ya tofauti za kiitikadi, na wakahimiza ujenzi wa jamii yenye misingi ya maadili, mawasiliano ya wazi, na ushirikiano wa kweli.
Katika mazungumzo hayo ya wazi na ya kiukweli, pande zote ziliweka wazi nia yao ya kuendeleza mashauriano ya mara kwa mara kwa ajili ya kulinda Umoja wa Waislamu, kukabiliana na changamoto za kijamii, na kuimarisha amani na utulivu katika jamii.
Kwa upande wake, Dkt. Ali Taqavi alieleza kuwa Taasisi ya Jamiat Al-Mustafa (s.a.w.w) inathamini sana jitihada za viongozi wa Kisunni nchini Tanzania katika kudumisha amani na mshikamano. Alisisitiza kwamba mazungumzo ya kielimu na ya kijamii baina ya Waislamu ni chachu ya maendeleo na msingi wa kuleta umoja wa Kiislamu duniani.
Ziara hii ni muendelezo wa juhudi za kuimarisha mawasiliano kati ya Madhehebu mbalimbali za Kiislamu na kujenga jukwaa la pamoja la kuhudumia jamii ya Kiislamu nchini Tanzania.
Tumekuwekea hapa chini sehemu ya picha za tukio hili:
Your Comment