Kikao hiki kilikuwa na madhumuni ya kujadili maandalizi ya kuandaa hafla ya usomaji wa Qur’ani Tukufu katika uwanja wa michezo wa jiji la Tanga, na kililenga kushirikiana kwa karibu katika kuhakikisha tukio hilo linakuwa la mafanikio na lenye athari chanya kwa jamii ya Kiislamu na wananchi kwa ujumla.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Hojjat-ul-Islam wal-Muslimin, Dr. Ali Taqavi, Rais wa Jamiatul Mustafa (s) - Dar-es-salaam, Tanzania, akiambata na Dr. Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA), walifanya Ziara muhimu katika jiji la Tanga.
Katika Ziara hii, walipata fursa ya kufanya Kikao cha ukaribu na urafiki kilichosheheni mazungumzo muhimu na Mheshimiwa Mufti Mkuu wa Tanzania Dr.Abubakar Zubair bin Ally, pamoja na Sheikh wa Mkoa wa Tanga kwa madhumuni ya kujadili maandalizi ya kuandaa hafla ya usomaji wa Qur’ani Tukufu katika uwanja wa michezo wa jiji la Tanga.
Kikao hicho kililenga kushirikiana kwa karibu katika kuhakikisha tukio hilo linakuwa la mafanikio na lenye athari chanya kwa jamii ya Kiislamu na wananchi kwa ujumla.
Your Comment