Lengo kuu la ziara hii lilikuwa ni kutathmini hali ya elimu katika shule hizo, na kujadili fursa za ushirikiano hasa katika eneo la kufundisha wa Elimu za Qur'an Tukufu na Sayansi za Kidini kwa ujumla.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Tarehe [07-05-2025], Hojjat al-Islam wal-Muslimin Dr.Ali Taqavi alifanya ziara katika shule za Abu al-Fadhl al-Abbas, Shule ya al_Mustafa, na Shule ya Qaem zilizopo katika jiji la Tanga.
Katika ziara hii, kulifanyika vikao na wakuu wa shule, walimu na maafisa wa elimu.
Lengo kuu la ziara hii lilikuwa ni kutathmini hali ya elimu katika shule hizo, na kujadili fursa za ushirikiano hasa katika eneo la ufundishaji wa Elimu za Qur'an Tukufu na Maarifa yote ya Kiislamu kwa ujumla.
Katika mkutano na walimu, zilijadiliwa mbinu za ufundishaji, rasilimali za kielimu zilizopo, pamoja na changamoto zinazowakabili walimu na wanafunzi.
Wakuu wa shule pia waliwasilisha taarifa kuhusu hali ya sasa ya wanafunzi, mipango inayoendelea, na malengo ya baadaye.
Walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali, hususan katika suala la Sayansi ya Kidini.
Mwisho wa ziara, mapendekezo mbalimbali yalitolewa kuhusu namna ya kuboresha mfumo wa elimu, kuinua ujuzi wa walimu, na kuongeza vifaa vya kujifunzia na kufundishia.
Your Comment