Mazungumzo yalijikita katika masuala muhimu ya kitaaluma, ikiwa ni pamoja na njia bora za kuimarisha elimu, kuinua viwango vya ufaulu, na kueneza Sayansi za Ahlul-Bayt (as). Aidha, walijadili namna ya kuimarisha ushirikiano na mshikamano baina ya taasisi za kielimu kwa lengo la kukuza maarifa ya Kiislamu na maadili mema kwa vijana.

8 Mei 2025 - 14:28

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA -Dkt. Ali Taqavi amefanya ziara muhimu na ya kihistoria katika Shule ya Kidini ya Mustafa iliyopo jijini Tanga, Tanzania. Katika ziara hiyo, Dkt. Taqavi alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo ya kina na viongozi pamoja na walimu wa shule hiyo.

Dkt. Ali Taqavi Afanya Ziara Muhimu katika Shule ya Mustafa, Tanga – Tanzania + Picha

Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala muhimu ya kitaaluma, ikiwa ni pamoja na njia bora za kuimarisha elimu, kuinua viwango vya ufaulu, na kueneza Sayansi za Ahlul-Bayt (as).

Aidha, walijadili namna ya kuimarisha ushirikiano na mshikamano baina ya taasisi za kielimu kwa lengo la kukuza maarifa ya Kiislamu na maadili mema kwa vijana.

Ziara hii imetajwa kuwa ya mafanikio makubwa, ikionyesha dhamira ya kweli ya kuendeleza elimu na kuimarisha ushirikiano wa kielimu katika jamii.

Your Comment

You are replying to: .
captcha