Katika kufunga kikao hicho, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum aliwapongeza viongozi wa Tanga kwa juhudi zao na kuwasihi waendelee kuwa mfano wa kuigwa katika kulinda na kuendeleza maelewano na utulivu wa kijamii. Viongozi wa Mkoa wa Tanga walieleza kufurahishwa kwao na ujio huo na kuahidi kutekeleza maazimio yaliyofikiwa kwa bidii na uwazi.
Shirika la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA), Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum, akiambatana na Dkt. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s) – Dar es Salaam, walifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania zilizopo katika Mkoa wa Tanga.
Katika ziara hiyo, viongozi hao walikutana na viongozi wa Jumuiya ya Mkoa wa Tanga kwa lengo la kubadilishana mawazo, kuimarisha mshikamano wa Jumuiya, na kujadili namna bora ya kuendeleza juhudi za kukuza maridhiano, amani, na mshikamano wa kitaifa.
Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni pamoja na:
Mikakati ya kueneza elimu ya amani na maridhiano katika jamii kupitia semina, makongamano, na warsha.
Ushirikiano wa Kitaifa na kimataifa katika kuimarisha maadili, ustawi wa jamii, na mafunzo ya kijamii kupitia taasisi za kielimu kama Jamiat Al-Mustafa(S) na kadhalika.
Changamoto zinazoikabili Jumuiya katika maeneo mbalimbali na njia za kuzitatua kwa ushirikiano wa karibu kati ya viongozi wa kitaifa na wa mikoa.
Kujenga misingi ya maelewano baina ya waumini wa dini tofauti ili kukuza umoja wa kitaifa.

Your Comment