Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Katika hali ya furaha na mshikamano wa kiroho, Hawza ya Wasichana iliyopo Kigamboni, Jijini Dar-es-Salaam, imeandaa hafla maalum ya kuadhimisha Usiku wa Kuzaliwa kwa Imam Ali bin Musa ar-Ridha (a.s), Imam wa nane katika silsila ya Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s).

8 Mei 2025 - 22:07

Hafla hiyo iliyofanyika usiku wa leo tarehe (08 -05- 2025), ilihudhuriwa na Wanafunzi wa Hawza hiyo ya Hazrat Zainab (sa), Walimu, Wazazi pamoja na waalikwa kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar-es-Salaam.

Maadhimisho ya Usiku wa Kuzaliwa kwa Imam Reza (a.s) Yafanyika katika Hawza ya Wasichana, Kigamboni, Dar-es-Salaam + Picha

Tukio hilo lilijawa na furaha, mawaidha, qaswida na mashairi ya kumsifu Imam Ridha (a.s), na lilikuwa na lengo la kuendeleza ufuasi na mapenzi kwa kizazi kitukufu cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) sambamba na kuhamasisha elimu na maadili ya Kiislamu miongoni mwa mabinti wa Kiislamu.

Katika hotuba yake, Mrs. Taqavi, Mkuu wa Hawza hiyo alisisitiza umuhimu wa kuiga Maisha ya Imam Ridha (a.s), hasa katika nyanja za elimu, uvumilivu na uadilifu. Aidha, alisisitiza jukumu la Wasichana wa Kiislamu katika kujifunza Dini yao kwa kina na kuwa Mabalozi wa amani na maadili mema katika jamii.

Wanafunzi wa Hawza walishiriki kikamilifu kwa kusoma Mashairi, kutoa Qaswida, na kufanya maigizo mafupi yanayoonesha historia ya maisha ya Imam Reza (a.s). Hafla ilihitimishwa kwa dua na zawadi kwa washiriki mbalimbali.

Maadhimisho haya yameonesha wazi dhamira ya kuendeleza turathi za Ahlul-Bayt (a.s) na kukuza ari ya kielimu kwa mabinti wa Kiislamu katika jamii ya Kiislamu hapa Tanzania.

Maadhimisho ya Usiku wa Kuzaliwa kwa Imam Reza (a.s) Yafanyika katika Hawza ya Wasichana, Kigamboni, Dar-es-Salaam + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha