Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Dua maalum ya Kitaifa kwa ajili ya kuwaombea rehema na maghfira Wanazuoni, Masheikh na watu mashuhuri wa Kiislamu waliotangulia mbele ya haki imefunguliwa leo, Alhamisi, tarehe 08 Mei, 2025, katika hafla iliyojaa heshima na unyenyekevu wa kiroho.

8 Mei 2025 - 23:09

Dua ya Kitaifa kwa ajili ya Kuwaombea Wanazuoni, Mashekhe na Watu Mashuhuri Waliotangulia Mbele ya Haki + Picha

Hafla hiyo imefunguliwa rasmi na Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo tukufu.

Dua ya Kitaifa kwa ajili ya Kuwaombea Wanazuoni, Mashekhe na Watu Mashuhuri Waliotangulia Mbele ya Haki + Picha

Dua hii itaendelea kwa siku ya Ijumaa (09 Mei, 2025) na kufikia hitimisho Jumamosi, tarehe 10 Mei, 2025, ikiwakutanisha waumini, viongozi wa dini, masheikh pamoja na jamii kwa ujumla kwa lengo la kuenzi mchango wa wale waliotangulia mbele ya Haki, na kumuomba Allah (s.w.t) awarehemu na kuwapokelea katika daraja za juu Peponi.

Dua ya Kitaifa kwa ajili ya Kuwaombea Wanazuoni, Mashekhe na Watu Mashuhuri Waliotangulia Mbele ya Haki + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha