Baada ya Swala ya Ijumaa, Dua ya Kitaifa iliendelea katika Msikiti huu. Viongozi wa Dini, Masheikh na Masheikhat wamehudhuria katika Dua hii, na Masheikhat waliwaongoza akina mama wa Kiislamu katika mihadhara na maombi maalum, ambayo yatadumu hadi wakati wa Swala ya Magharibi.

9 Mei 2025 - 15:15

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA – Swala ya Ijumaa, leo hii 9 Mei, 2025 – Jijini Dar –es- Salaam, imeswaliwa katika Msikiti wa Kisasa wa Mfalme Mohammed VI uliopo Makao Makuu ya BAKWATA, ambapo imeongozwa na Samahat Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt.Abubakar Zubair bin Ally, akiwashirikisha:

  • Masheikh kutoka Mikoa yote,
  • Masheikh wa Wilaya mbalimbali,
  • Viongozi wa Taasisi za Kiislamu kutoka kila pembe ya nchi.

Baada ya Swala ya Ijumaa, Dua ya Kitaifa iliendelea katika Msikiti huu. Viongozi wa Dini, Masheikh na Masheikhat wamehudhuria katika Dua hii, na Masheikhat waliwaongoza akina mama wa Kiislamu katika mihadhara na maombi maalum, ambayo yatadumu hadi wakati wa Swala ya Magharibi.

Kesho - Jumamosi

Kesho ni kilele cha Dua ya Kitaifa ya Siku Tatu, ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.

Taarifa hii ni kwa hisani kubwa ya:
Dkt. Harith Nkussa
Msemaji Maalum wa Mufti wa Tanzania.

🕌 Swala ya Ijumaa – Msikiti wa Mfalme Mohammed VI, Bakwata Makao Makuu + Picha

Tumekuwekea hapo chini picha zaidi za tukio hili

Your Comment

You are replying to: .
captcha