Sheikh Khamis, Khatibu wa Swala ya Ijumaa, aliwakumbusha waumini kuwa Imam Ridha (a.s) alikuwa mfano wa huruma, elimu, subira na ukarimu, na kwamba alisimama imara kwa ajili ya haki na ustawi wa binadamu wote, bila kubagua kwa dini, rangi au kabila.

9 Mei 2025 - 23:41

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Leo, Ijumaa, 9 Mei, 2025, Waumini wa Kiislamu wamekusanyika kwa ajili ya ibada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Zayn al-Abidin (a.s) nchini Burundi, ambapo Khutba ya leo iliyotolewa na Kahtibu, Sheikh Khamis Sadiq ilijikita katika kumuenzi Imam Ali bin Musa al-Ridha (a.s.), Mtukufu na Mkarimu wa Kizazi Kitukufu cha Mtume Muhammad (s.a.w.w.), huku maandalizi ya Waislamu wote ndani ya nchi wenye Mapenzi na Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w) yakiendelea kufanyika kuelekea Kusherehekea Siku ya Kuzaliwa Kwake.

Khutba ya Ijumaa Yamuadhimisha Imam Ali bin Musa al-Ridha (a.s.) – Msikiti wa Imam Zayn al-Abidin, Burundi + Picha

Khutba hiyo ya Swala ya Ijumaa, iliyoongozwa na Sheikh Khmis Sadiq, ilisisitiza nafasi ya Imam Ridha (a.s.) katika Uislamu, kwamba sio tu alikuwa ni Kiongozi wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashari, bali pia alikuwa “tumaini la wanyonge na nuru ya wenye huzuni na maumivu duniani kote.”

Sheikh Khamis, Khatibu wa Swala ya Ijumaa, aliwakumbusha waumini kuwa Imam Ridha (a.s) alikuwa mfano wa huruma, elimu, subira na ukarimu, na kwamba alisimama imara kwa ajili ya haki na ustawi wa binadamu wote, bila kubagua kwa dini, rangi au kabila.

“Kuzaliwa kwa Imam Ridha (a.s.) ni ishara ya huruma ya Mwenyezi Mungu ambayo huvuka mipaka ya kisiasa na ya kidini. Alikuwa ni faraja kwa walio na huzuni na mtetezi wa waliodhulumiwa,” alisema Sheikh Khamis Sadiq.

Aidha, Sheikh Khamis Sadiq, aliwahimiza waumini kuiga mwenendo wa Imam huyo mwema (as), kwa kusimama dhidi ya dhulma na kuwahudumia wanyonge kama njia ya kuendeleza nuru ya Ahlul-Bayt (a.s).

Khutba hiyo pia ilitoa wito kwa jamii ya kimataifa kumtambua Imam Ridha (a.s) kama hazina ya kiroho kwa binadamu wote, na si kwa Waislamu wa Shia pekee. Sheikh Khamis alisisitiza kuwa mapenzi na heshima kwa viongozi wa haki ni wajibu wa kila mtu anayetamani uadilifu na maadili mema.

Waumini walihitimisha ibada hiyo kwa maombi na salamu kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake(as), wakiomba baraka, neema na taufiki ya kuweza kuiga sira ya Imam Ridha (a.s) katika maisha yao ya kila siku.

Khutba ya Ijumaa Yamuadhimisha Imam Ali bin Musa al-Ridha (a.s.) – Msikiti wa Imam Zayn al-Abidin, Burundi + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha