Majlis ya Khitma iliongozwa na Samahat Sheikh Hemed Jalala, ambapo kisomo maalumu cha Qur'an na dua za kumuombea rehema Marhuma Fatma Mwiru zilisomwa kwa unyenyekevu na taadhima.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA -Majlis ya Arbaeen kwa ajili ya kumuenzi na kumrehemu Marhuma Bibi Fatma Mwiru imefanyika kijijini kwao Kimani, katika Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani.
Miongoni mwa Masheikh na Viongozi wa Dini waliohudhuria ni:
-
Dr. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s), Dar es Salaam, Tanzania.
-
Sayyid Arif Naqvi, Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Hojjat al-Asr Foundation of Tanzania
-
Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna Ashari Tanzania (T.I.C).
Majlis ya Khitma iliongozwa na Samahat Sheikh Hemed Jalala, ambapo kisomo maalumu cha Qur'an na dua za kumuombea rehema Marhuma Fatma Mwiru zilisomwa kwa unyenyekevu na taadhima.
Your Comment