Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Mnamo tarehe 9/5/2015, wanafunzi wa Hawzatul-Qaim walishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika katika Kata ya Ngamiani Kaskazini, Jiji la Tanga. Tukio hili muhimu lilifanyika kwa lengo la kuimarisha usafi wa mazingira pamoja na kuonyesha mshikamano kati ya Taasisi za Dini na Serikali za mitaa katika kujenga jamii safi na salama.

11 Mei 2025 - 15:24

Wanafunzi wa Hawzatul-Qaim walishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika katika Kata ya Ngamiani Kaskazini, Jiji la Tanga + Picha

Wanafunzi hao waliongozwa na Mudir wa Hawzatul-Qaim, Sheikh Kadhim Abbas, ambaye alitoa msukumo mkubwa katika ushiriki wa vijana wa Kiislamu katika shughuli za kijamii.

Kwa upande wa Serikali, tukio hili lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa eneo hilo akiwemo:

  1. Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Ngamiani Kaskazini.

  2. Mtendaji wa Kata ya Ngamiani Kaskazini.

  3. Afisa wa Afya wa Kata.

  4. Mwenyekiti wa Mtaa wa Lumumba, mtaa ambao pia ndio makazi ya Hawzatul-Qaim (as).

Viongozi wengine wa Serikali na jamii walihudhuria kuonyesha mshikamano wao na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za kijamii na kimaendeleo.

Tukio hili limefanikishwa kwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali ya mitaa, Hawzatul-Qaim (as), na Taasisi ya Bilal Tanga kwa ujumla. Ushirikiano huu ni mfano bora wa namna taasisi za Dini zinavyoweza kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ya kijamii.

Mwisho, tunatoa shukrani zetu kwa washiriki wote na tunaamini kuwa shughuli kama hizi zitaendelea kuhamasishwa ili kulinda afya na mazingira ya wakazi wa Jiji la Tanga.

Your Comment

You are replying to: .
captcha