Tunaamini kuwa mwanamke anapopata elimu, jamii nzima hunufaika. Hii ni kwa sababu mwanamke ni nusu ya jamii, na mchango wake katika malezi, maadili, na maendeleo ya kijamii hauna kifani. Elimu ya mwanamke si chaguo bali ni hitaji muhimu kwa ustawi wa jamii.

18 Mei 2025 - 16:52

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Chuo cha Mabanati cha Hazrat Zainab (sa) ni taasisi ya kipekee inayotoa elimu safi ya Dini kwa mabinti wa Kiislamu nchini Tanzania. Kikiwa kimejikita katika maneneo ya Kigamboni, Jijini Dar es Salaam. Chuo hiki kina dhamira ya kuhakikisha kuwa mabinti wanapata maarifa sahihi ya kidini yanayowawezesha kujenga jamii imara, yenye maadili na heshima.

Mwanamke nusu ya Jamii | Sala ya Jamaa na Mawaidha ya Kiroho Katika Chuo cha Mabanati cha Hazrat Zainab (sa)
Kigamboni, Dar es Salaam + Picha

Tunaamini kuwa Mwanamke anapopata elimu, jamii nzima hunufaika. Hii ni kwa sababu mwanamke ni nusu ya jamii, na mchango wake katika malezi, maadili, na maendeleo ya kijamii hauna kifani. Elimu ya Mwanamke si chaguo bali ni hitaji muhimu kwa ustawi wa jamii.

Mwanamke nusu ya Jamii | Sala ya Jamaa na Mawaidha ya Kiroho Katika Chuo cha Mabanati cha Hazrat Zainab (sa)
Kigamboni, Dar es Salaam + Picha

Kupitia Sala ya Jamaa, mawaidha ya kiroho, na masomo ya kidini, chuo hiki kimekuwa nguzo muhimu ya kulea kizazi cha mabinti wenye maarifa, imani thabiti, na uchamungu. Tunahakikisha kwamba kila binti anayepitia chuo hiki anakuwa tayari kuwa kiongozi mwema katika familia yake na jamii kwa ujumla. Chuo cha Hazrat Zainab (sa) kipo kwa ajili ya kutimiza jukumu hili adhimu – kupitia kusambaza elimu na maarifa safi ya Kiislamu kwa mabinti wa Kitanzania.

Mwanamke nusu ya Jamii | Sala ya Jamaa na Mawaidha ya Kiroho Katika Chuo cha Mabanati cha Hazrat Zainab (sa)
Kigamboni, Dar es Salaam + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha