Wasomaji Bingwa wa Qur’an Tukufu kutoka Iran Watua Tanzania kwa Kisomo Maridhawa cha Tajweed + Picha
Kisomo hicho kitafanyika kuanzia kesho, tarehe 20 Mei 2025, katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wasomaji bingwa na mashuhuri wa Kimataifa wa Qur’an Tukufu kwa njia ya Tajweed kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamewasili leo hii nchini Tanzania kwa ziara maalum ya Kisomo cha Qur'an Tukufu kwa njia ya Tajweed kitachogusa nyoyo za wapenzi wa Qur’an.
Kisomo hicho kitafanyika kuanzia kesho, tarehe 20 Mei 2025, katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Muda: Kuanzia saa 8:00 kamili mchana hadi saa 11:00 jioni.
Wapenzi na waumini wa Qur’an Tukufu mnakaribishwa kwa wingi kushiriki katika tukio hili adhimu lenye baraka na fursa ya kujifunza usomaji wa Qur’an kwa lafudhi sahihi na ufasaha wa Tajweed kutoka kwa wasomaji wa kiwango cha juu duniani.
Usikose Kuhudhuria!
Your Comment