Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mh. Balozi wa Iran nchini Tanzania akiwa pamoja na MKurugenzi kituo cha utamaduni ubalozi wa Iran Dr. Marif, na Rais wa Jamiat Al-Mustafa International University -Tanzania, Dr.Ali Taqavi, wameongoza mapokezi ya wageni kumi wakiwemo wasomaji Qur-an watano ambao watashiriki makongamano ya Qur-an Tukufu, Jijini Dar es salaam na Tanga.
19 Mei 2025 - 21:25
News ID: 1690631

Kongamano la kwanza litafanyika kesho Jumanne ukumbi wa Mwalimu Nyerere katikati ya jiji la Dar es salaam na Kongamano lingine uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga na Kongamano la mwisho litafanyika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Habari hii imekujieni kwa hisani kubwa ya:
Dr. Harith Nkussa.
Msemaji Maalum wa Mufti.
Dar es salaam - Tanzania.
Your Comment