Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Uislamu umesisitiza sana juu ya umuhimu wa kujifunza na kufundisha Qur’an Tukufu. Qur’an si tu kitabu cha kusomwa, bali ni mwongozo wa maisha ya kila siku kwa Muislamu. Inatufundisha maadili, ibada, uhusiano mwema kati ya watu, na jinsi ya kumtii Mwenyezi Mungu katika kila nyanja ya maisha.
20 Mei 2025 - 13:51
News ID: 1690838
Kumfundisha mtu Qur’an ni ibada yenye thawabu kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu. Mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema:
“Aliyebora kati yenu ni yule anayejifunza Qur’an na akawafundisha wengine.”
Hivyo basi, jukumu la kufundisha Qur’an si la kawaida - Bali ni kazi tukufu inayosaidia kusambaza nuru ya uongofu wa Mwenyezi Mungu Duniani.
Your Comment