Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Daniel Baran Sillo, ambaye katika hotuba yake aliwapongeza waandaaji na washiriki, huku akisisitiza nafasi ya Qur’an katika kuleta umoja, maadili na maendeleo ya Taifa.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Himidi zote na kila sifa Njema ni zake Mwenyezi Mungu aliyejalia Kongamano la 30 la Qur’an Tukufu kufanyika kwa mafanikio makubwa Jijini Dar-es-Salaam - Tanzania, likiwakutanisha wasomaji mahiri wa Qur’an kutoka nchini Iran na ndani ya Tanzania, likiwa ni jukwaa la kukuza uelewa wa mafundisho ya Qur’an na kuimarisha mshikamano wa Kiislamu katika jamii.
Kongamano hili liliandaliwa kwa ushirikiano wa taasisi mbalimbali zikiwemo: Jamiat al-Mustafa (s) tawi la Tanzania chini ya uongozi wa Hojjatul Islam wal Muslimin, Dr. Ali Taqavi, Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Taifa, Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) likiwa chini ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dr. Abubakar Zubair bin Ally, pamoja na Kitengo cha Utamaduni wa Iran kinachoongozwa na Dr. Maarifi.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa: Daniel Baran Sillo, ambaye katika hotuba yake aliwapongeza waandaaji na washiriki, huku akisisitiza nafasi ya Qur’an katika kuleta umoja, maadili na maendeleo ya Taifa.
Akizungumza katika Kongamano hilo, Dr. Ali Taqavi aliwahimiza waumini wa Kiislamu kuendeleza juhudi za kusoma na kuelewa Qur’an kwa kina, kwa ajili ya kuleta Amani, Umoja Mshikamano na Ustawi wa Jamii ya Mwanadamu.
Tukio hili la kiroho limeendelea kuthibitisha nafasi ya Qur’an Tukufu kama dira ya maisha ya kijamii na kiroho, huku likiwa ni ishara ya mshikamano na ushirikiano miongoni mwa Waislamu ndani na nje ya Tanzania.
Your Comment