Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika hafla ya kipekee iliyofanyika pembezoni mwa Kongamano la 30 la Qur'an Tukufu, lililofanyika jana, tarehe 20 Mei 2025, katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, Tanzania — Tafsiri mpya ya Qur’an Tukufu kwa lugha ya Kiswahili imezinduliwa rasmi.
Tafsiri hii mpya iliyotafsiriwa (Tarjumiwa) kwa Lugha ya Kiswahili, inayojulikana kwa jina "Tafsiri Nur", imeandikwa na: Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhsin Qiraati, na lugha yake ya awali ni Kiajemi. Sasa, Tafsiri hiyo imepatikana kwa lugha fasaha ya Kiswahili baada ya kutarjumiwa kwa ufanisi mkubwa na Sheikh Dr. Baqir Matega.
Uzinduzi huu unachukuliwa kuwa hatua muhimu katika kusambaza maarifa ya Qur’an kwa wasemaji wa Kiswahili, na unalenga kuwapa waumini wa Kiislamu uelewa mpana na wa kina wa mafundisho ya Kitabu hiki Kitukufu kwa lugha wanayoifahamu vizuri.
Your Comment