Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Wanafunzi wa Hawzat Imam Ridha (as) leo hii wamehudhuria darasa la Akhlaq pamoja na kupokea nasaha kutoka kwa Sheikh Shaabani Kashakali mara baada ya swala ya Dhuhrain. Katika darasa hilo, Sheikh alisisitiza umuhimu wa kujipamba na maadili mema, kudumisha ikhlasi katika elimu, na kujiepusha na sifa mbaya kama kiburi na hasadi.
22 Mei 2025 - 23:22
News ID: 1691681
Pia aliwahimiza wanafunzi kuwa wawakilishi bora wa Uislamu katika jamii kwa mwenendo na tabia zao, akisema:
“Elimu bila maadili ni kama taa bila mafuta - Haiwezi kuangaza.”
Darasa lilihitimishwa kwa dua na wasia wa kuongeza juhudi katika kujisafisha nafsi pamoja na kutenda kwa mujibu wa elimu wanayoipata.
Your Comment