Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (A.S) - ABNA- Limeripoti kufanyika kwa Majlisi ya Maombolezo ya Shahadat ya Imam Jawad (as) yenye hisia kubwa nchini Burundi.

27 Mei 2025 - 17:53

Burundi | Maombolezo ya Kuuawa Shahidi kwa Imam Muhammad Al-Jawad (A.S) Yafanyika kwa Hisia Kubwa

Leo hii, tarehe: 27 Mei, 2025 - Katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa Shahidi kwa Imam Muhammad Al-Jawad (A.S), Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (A.S) - ABNA- Limeripoti kufanyika kwa Majlisi ya Maombolezo ya Shahadat ya Imam Jawad (as) yenye hisia kubwa nchini Burundi. 

Hafla hiyo imeandaliwa katika Shule ya Imam Zainul Abidin (A.S), ambapo Wapenzi na Wafuasi wa Ahlul Bayt (A.S) wamejitokeza kwa wingi kushiriki kwenye Majlisi hiyo takatifu.

Kikao hicho kimejumuisha maombolezo, mawaidha na mashairi ya huzuni, sambamba na mjadala wa kielimu kuhusu maisha ya Imam Muhammad Al-Jawad (A.S). 

Sehemu ya kikao hicho imejikita katika kuchambua nukta muhimu kutoka katika kitabu “Mwanadamu wa Miaka 250” – ambacho ni mkusanyiko wa hotuba za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Sayyid Ali Khamenei, kuhusu maisha ya Maimamu wa Ahlul-Bayt (A.S).

Mjadala huo umeangazia kwa kina mtazamo wa makusudi na wa kiroho juu ya maisha ya Maimamu Maasumina (A.S) - hususan Imam Jawad (as) -  ukionyesha nafasi yao katika uongozi wa Umma na jitihada zao za kulinda mafundisho sahihi ya Uislamu katika mazingira magumu ya kisiasa.

Mahudhurio makubwa ya Waumini katika Kikao hiki si tu kwamba yametoa faraja na mshikamano wa kiroho, bali pia yametoa ushahidi wa dhahiri kuwa Majlisi za kuwakumbuka Maimamu wa Kizazi cha Mtume (S.A.W.W) ni sehemu muhimu ya ibada na kujenga Umoja wa Waumini.

Tukio hili limeacha athari ya kiroho na kielimu, na kuendelea kuimarisha Mapenzi ya Umma kwa Maimamu Watukufu wa Ahlul-Bayt (A.S).

Burundi | Maombolezo ya Kuuawa Shahidi kwa Imam Muhammad Al-Jawad (A.S) Yafanyika kwa Hisia Kubwa

Your Comment

You are replying to: .
captcha