Katika kumbukumbu ya siku ya kuuawa Shahidi kwa Imam Muhammad al-Jawad (A.S.), Mkurugenzi wa Shule hii ya Mabanati, alitoa Hotuba Maridhawa, ambapo alizungumzia mambo yafuatayo: Alianza kwa kutaja siku ya kuzaliwa kwa Imam al-Jawad (A.S.) na sifa maalumu za Imam huyo wa tisa, namna alivyopata shahada, pamoja na hadithi mbalimbali na nzuri zilizopokelewa kutoka kwake.

27 Mei 2025 - 18:32

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Ifuatayo ni taarifa ya Hafla ya Kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Kuuawa Shahidi kwa Imam Muhammad al-Jawad (A.S.), iliyofanyika leo hii, tarehe: 27/5/2025, Siku ya Jumanne Katika Hawza ya Wasichana ya Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni, Dar-es-salaam - Tanzania.

Majlisi ya Kumbukumbu ya Shahada ya Imam al-Jawad (A.S.) Yafanyika katika Hawzat ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa), Kigamboni - Dar es Salaam + Picha

Mzungumzaji katika Majlisi hii: Mkurugenzi wa Hawzat ya Wasichana, Bi. Haja Taqavi.

Katika kumbukumbu ya siku ya kuuawa Shahidi kwa Imam Muhammad al-Jawad (A.S.), Mkurugenzi wa Shule hii ya Mabanati, alitoa Hotuba Maridhawa, ambapo alizungumzia mambo yafuatayo:  Alianza kwa kutaja siku ya kuzaliwa kwa Imam al-Jawad (A.S.) na sifa maalumu za Imam huyo wa tisa, namna alivyopata shahada, pamoja na hadithi mbalimbali nzuri zilizopokelewa kutoka kwake.

Miongoni mwa hadithi hizo ni:
"Mu’min anahitaji sifa tatu: Taufiki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mhubiri wa nafsi yake mwenyewe, na kuukubali ushauri kutoka kwa anayemnasihi." Kisha alitoa ufafanuzi wa hadithi hii kwa wanafunzi waliohudhuria katika Majlis hii Tukufu.

Hadithi nyingine kutoka kwa Imam al-Jawad (A.S.) aliyoinukuu ni:
"Yeyote atakayejiona hana haja kwa yeyote ispokuwa ni mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu tu, basi huyo watu ndio watahitajia kwake."

Hafla hii ilihitimishwa kwa dua, kusoma salawat, na kusomwa kwa Surat al-Fatiha na kuzitoa hadia (zawadi) thawabu zake kwa Imam al-Jawad (A.S).

Majlisi ya Kumbukumbu ya Shahada ya Imam al-Jawad (A.S.) Yafanyika katika Hawzat ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa), Kigamboni - Dar es Salaam + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha