Maadhimisho ya Wafat wa Imam Muhammad al-Jawad (as) – Dar es Salaam, Tanzania

27 Mei 2025 - 23:58

Maadhimisho ya Wafat wa Imam Muhammad al-Jawad (as) – Dar es Salaam, Tanzania

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Wanafunzi wa Al-Mustafa International Foundation tawi la Dar-es-Salaam, Tanzania, wameshiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Kishahidi cha Imam wa tisa katika silsila ya Maimamu wa Kizazi Kitukufu cha Mtume Muhammad (saww), Imam Muhammad al-Jawad (as).

Maadhimisho ya Wafat wa Imam Muhammad al-Jawad (as) – Dar es Salaam, Tanzania

Mzungumzaji katika Majlis hiyo alikuwa Sheikh Bakari Mtulia, ambaye alitoa hotuba yenye kuelimisha kuhusu maisha na sifa za kipekee za Imam al-Jawad (as). Alielezea hekima, elimu, na ucha Mungu aliopambika nao Imam huyu tangu akiwa na umri mdogo.Sheikh Mtulia pia alieleza kwa uchungu njama zilizofanywa na maadui wa Ahlul Bayt (as), ambazo zilimpelekea Imam kuuawa kwa sumu kupitia kwa mke wake aliyeitwa Ummul Fadhl, binti ya Khalifa Abbasiy, Al-Ma'mun.

Maadhimisho ya Wafat wa Imam Muhammad al-Jawad (as) – Dar es Salaam, Tanzania

Njama hizo zilitokana na chuki ya kisiasa na kidini dhidi ya nafasi na elimu ya Imam katika jamii.

Katika hitimisho la hotuba yake, Sheikh Mtulia alisisitiza umuhimu wa kushikamana na mafunzo safi na yenye hekima aliyotuachia Imam al-Jawad (as), ambayo yanabaki kuwa dira ya haki, uadilifu na uongofu kwa Waislamu na jamii nzima.

Maadhimisho ya Wafat wa Imam Muhammad al-Jawad (as) – Dar es Salaam, Tanzania

Your Comment

You are replying to: .
captcha