Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Falah Islamic Foundation imeandaa programu maalum kwa ajili ya vijana kwa lengo la kuwawezesha kielimu katika masuala ya ujasiriamali na kujiajiri. Kupitia programu hii, vijana wamepewa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutumia maarifa hayo kama nyenzo ya kuboresha maisha yao ya kila siku.
28 Mei 2025 - 13:33
News ID: 1693451
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika darsa hiyo ni:
1_Jinsi ya kutengeneza sabuni na mafuta mbalimbali.
2_Mafunzo ya upishi bora wa vyakula.
3_Elimu ya msingi kuhusu ujasiriamali na mbinu za kujiajiri.
Lengo kuu la Falah ni kuwahamasisha vijana wajitegemee na kuwa chachu ya maendeleo katika jamii zao.
Shukran sana.
Your Comment