Wakati wa ziara hiyo, wageni walikutana na wanafunzi na viongozi wa hawza, ambapo walitoa nasaha muhimu kuhusu umuhimu wa kusoma kwa bidii, kuwa na subira, uvumilivu, na unyenyekevu katika njia ya elimu ya dini.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tarehe 28 Mei 2025, Hawza ya Imam Swadiq (as) iliyopo Kigogo Post, Dar-es-Salaam, chini ya usimamizi wa Samahat Sheikh Hemed Jalala, ilipokea ugeni kutoka Maktaba ya Sayyid Hakim (ra) ya Najaf Ashraf, Iraq.
Ugeni huo uliongozwa na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Thamir na ulipokelewa kwa mapokezi mazuri.
Wakati wa ziara hiyo, wageni walikutana na wanafunzi na viongozi wa hawza, ambapo walitoa nasaha muhimu kuhusu umuhimu wa kusoma kwa bidii, kuwa na subira, uvumilivu, na unyenyekevu katika njia ya elimu ya dini.
Wageni walikumbusha kuwa kila mwanafunzi ana wajibu mkubwa mbele ya jamii yake, na anapaswa kutambua dhamana hiyo tangu mwanzo wa safari yake ya kielimu.
Aidha, kikao maalum kilifanyika kati ya viongozi wa hawza na wageni hao, ambapo taratibu za kiidara za hawza hiyo zilifafanuliwa kwa wageni. Ziara hiyo ilileta hamasa na mafundisho muhimu kwa wanafunzi wa hawza hiyo.
Your Comment