Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa fadhila na rehema za Mwenyezi Mungu na kwa juhudi za pamoja za dada zetu waaminifu na wachapa kazi katika Chuo cha Dini cha Hazrat Zaynab (S.A), mradi wa ujenzi na maandalizi ya kituo cha masomo kwa Mabinti wa Kiislamu sasa umekamilika kwa ukamilifu.
Mradi huu ulihusisha hatua mbalimbali kama vile ujenzi, upakaji rangi, urembo wa mazingira, pamoja na ukamilishaji wa huduma na vifaa vya kiufundi - na sasa kituo hiki kiko tayari kwa matumizi rasmi.
Sambamba na kukamilika kwa mradi huu, dada zetu wa chuo, kwa moyo wa jihadi na kwa lengo la kuunda mazingira yenye uhai na mafanikio, wameanzisha shughuli za kilimo katika eneo la jirani na jengo la kituo hicho cha Wanafunzi wa Kike.
Shughuli hizi zinajumuisha upandaji wa mazao mepesi ya kilimo, upandaji wa maua, na uanzishaji wa mandhari ya kijani kwa kutumia rasilimali zilizopo - yote haya yakifanywa kwa juhudi binafsi za Wanafunzi wa chuo.
Tumekuwekea hapo chini mfululizo wa picha zinazoonyesha sura ya mwisho ya mradi pamoja na shughuli za kilimo za dada zetu ambao ni Wanafunzi wa Chuo hiki.
Your Comment