Baada ya kuja kwa Mtume wa Uislamu (S.A.W.W), Hadhi ya Mwanamke ilipandishwa kwa kiwango kikubwa. Mfano wa wazi ni Malezi ya Bibi Fatima Zahra (S.a) aliyolelewa na Mtume mwenyewe(S.A.W.W), na kuwa kigezo bora kwa Waislamu wote.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo Ijumaa - Tarehe: 30/5/2025 - Swala ya Jamaa ya Adhuhuri na Alasiri imeswaliwa katika Hawzat ya Mabinti ya Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni, Dar-es-salaam.
Idadi ya Washiriki katika Sala hii ya Jamaa: Wanafunzi wote - 150. Imam wa Sala: Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ghawth.
Baada ya kuswali Swala ya Adhuhuri na Alasiri kwa Sura ya Jamaa, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ghawth alitoa Hotuba Maridhawa kuhusu umuhimu wa Tabligh (Uhubiri au Kueneza mafunzo ya Dini Tukufu ya Kiislamu) na ushirikiano wa kijamii. Katika Hotuba hiyo, alisisitiza kuwa Wanawake wa Kiislamu wanayo nafasi muhimu na ya msingi katika kueneza Dini.
Katika hotuba yake, alirejelea enzi za Ujahili (au Ujahiliyya: Zama za Kabla ya Uislamu) ambapo Mabinti walikuwa wakizikwa wakiwa hai. Mwanamke aliyeumbwa kwa Hadhi na Heshima, alikuwa akipokonywa Hadhi yake kabla ya Uislamu.
Hata hivyo, kwa kuja kwa Mtume wa Uislamu (S.A.W.W), Hadhi ya Mwanamke ilipandishwa kwa kiwango kikubwa.
Mfano wa wazi ni Malezi ya Bibi Fatima Zahra (SA) aliyolelewa na Mtume mwenyewe(S.A.W.W), na kuwa kigezo bora kwa Waislamu wote.
Pia alieleza kuwa Mtume Muhammad (S.A.W.W) kwa tabia na mwenendo wake alitufundisha jinsi ya kuishi maisha bora - kuwa na maadili mema, upendo, uaminifu, na urafiki - na kutuepusha na tabia zote mbaya.
Hotuba hiyo ilipokelewa vizuri na Wanafunzi na ilijawa na hali ya kiroho na utulivu mkubwa.
Your Comment