Katika Khutba za Ijumaa, Imam alikumbusha kuwa: Kuswali Sala Al-Jum’a ni moja ya dalili za mshikamano wa Kiislamu na ni fursa ya kila wiki ya kuhuisha Ahadi ya kumtii Mwenyezi Mungu(SWT), pamoja na kuongeza uelewa wa Dini na Jamii katika mioyo ya Waumini.

30 Mei 2025 - 21:55

Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa msaada na nguvu za Mwenyezi Mungu, Taasisi ya "Hujjat al-Asr Society of Tanzania" imesimamisha Sala ya Jumu’a Tukufu au 'Sala ya Ijumaa' leo hii tarehe 30 Mei, 2025 katika Misikiti mbalimbali iliyoko katika maeneo tofauti ya nchi chini ya Usimamizi wa Taasisi hii ya Kiislamu.

Sala ni Nguzo ya Dini - Na Kuswali Sala ya Ijumaa ni Kuimarisha na Kuhuisha Ahadi na Mwenyezi Mungu + Picha

Katika Picha hizi, Imam alitoa Khutba mbili za Sala ya Ijumaa katika moja ya Husseiniyyah za Taasisi hiyo. Katika Khutba yake, alisisitiza umuhimu wa Sala kama nguzo kuu ya Dini, akibainisha kuwa ni msingi muhimu ambao imani haiwezi kukamilika bila kuzingatia Ibada na Sala kama hiyo. 

Aidha, alisisitiza kuwa kuswali Sala Al-Jum’a ni moja ya dalili za mshikamano wa Kiislamu na ni fursa ya kila wiki ya kuhuisha Ahadi ya kumtii Mwenyezi Mungu(SWT), pamoja na kuongeza uelewa wa Dini na Jamii katika mioyo ya Waumini.

Katika khutba yake, alielezea jukumu la Waumini kushiriki kikamilifu katika kufuata mafundisho ya Kiislamu kwa makini, hasa katika nyakati hizi za changamoto za Kidini na Maadili zinazowakumba baadhi ya watu katika jamii za kisasa. 

Sala ni Nguzo ya Dini - Na Kuswali Sala ya Ijumaa ni Kuimarisha na Kuhuisha Ahadi na Mwenyezi Mungu + Picha

Pia alisisitiza kuwa Misikiti inapaswa kubaki kama vuguvugu la mageuzi, na kitovu cha uelewa na ushirikiano wa kiroho na kitamaduni.

Kikao hicho cha Sala ya Ijumaa kilifanyika kwa hali ya msimamo wa kiroho, ambapo Waumini walijitokeza kwa wingi na kuonyesha Utulivu mkubwa katika kusikiliza ujumbe wa khutba ya Ijumaa, huku wakimuomba Mwenyezi Mungu awasaidie kudumu katika njia nzuri na iliyonyooka, na kuleta mafanikio katika maisha yao.

Your Comment

You are replying to: .
captcha