Sayyid Mansour Al-Musawiy alisisitiza kuhusu utukufu wa Mwezi wa Dhilhijja, hasa siku zake kumi za mwanzo ambazo zimepewa heshima kubwa katika mafundisho ya Kiislamu. Alieleza kuwa hizi ni siku adhimu ambazo Mwenyezi Mungu ameapa kwazo katika Qur'an Tukufu (Surat al-Fajr: 2 – "Na kwa masiku kumi!"), na kwamba ndani yake kuna fursa kubwa kwa Muumini kujikurubisha kwa Mola wake kwa kukithirisha Ibada kama vile: Kuswali sana, kusoma Qur'an, kufanya dhikri (kumkumbuka Mwenyezi Mungu) na kuomba dua mbalimbali.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, Tarehe 30 Mei, 2025, Swala ya Ijumaa imesimamishwa / imehuishwa katika Masjid ya Chuo Kikuu cha Kidini cha: Jamiatul Mustafa (s), Dar es Salaam – Tanzania. Imam na Khatibu wa Ijumaa: Sayyid Mansour Al-Musawiy.
Katika Swala ya Ijumaa ya leo, Sayyid Mansour Al-Musawiy aliiongoza Swala hiyo na baada ya kutoa Khutba mbili zenye ujumbe mzito na wa kuamsha hisia za kiroho kwa Waumini.
Mada ya Khutba:
"Fadhila za Mwezi wa Dhilhijja na Aamali Zake Muhimu"
Sayyid Mansour Al-Musawiy alisisitiza kuhusu utukufu wa mwezi wa Dhilhijja, hasa siku zake kumi za mwanzo ambazo zimepewa heshima kubwa katika mafundisho ya Kiislamu. Alieleza kuwa hizi ni siku adhimu ambazo Mwenyezi Mungu ameapa nazo katika Qur'an Tukufu (Surat al-Fajr: 2 – "Na kwa masiku kumi!"), na kwamba ndani yake kuna fursa kubwa kwa Muumini kujikurubisha kwa Mola wake.
Mambo Muhimu Aliyosisitiza:
-
1_Kukithirisha Ibada: Kuswali sana, kusoma Qur'an, kufanya dhikri (kumkumbuka Mwenyezi Mungu) na kuomba dua mbalimbali.
-
2_Siku ya Arafa: Ni siku ya malipo makubwa, na ni wakati wa kuomba haja na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
-
3_Kufunga: Kufunga siku za mwanzo za Dhilhijja, hasa siku ya Arafa kwa wasiokuwa Hujaji, kuna malipo makubwa.
-
4_Sadaka na Msaada: Kuwasaidia wahitaji katika kipindi hiki ni miongoni mwa ibada zinazopendwa sana.
-
5_Kumuomba Mwenyezi Mungu: Amesisitiza sana kutumia masiku haya kumuomba Allah atujalie haja zetu, atuondolee mashaka na kuturahisishia mambo yetu ya dunia na Akhera.
Sayyid Mansour alihitimisha kwa kuwakumbusha Waislamu kuwa maisha ya dunia ni ya mpito na ni jukumu letu kuchangamkia fursa hizi adhimu ili kujipatia radhi ya Mwenyezi Mungu.
Your Comment