Balozi wa Iran nchini Kenya, Dkt. Ali Gholampour, aliongoza Kikao hicho na kutoa hotuba kuu iliyomuenzi Imam Khomeini (MA) kama Kiongozi wa Mapinduzi na Mwanafalsafa wa Kiroho mwenye ushawishi mkubwa hadi leo hii.

1 Juni 2025 - 00:23

 Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wairani wanaoishi nchini Kenya wameungana na Wakenya siku ya Jumamosi katika Baraza la Kitamaduni la Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jijini Nairobi kuadhimisha miaka 36 tangu kufariki kwa Imam Khomeini(MA), Mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979.

Wairan Wanaishi Nchini Kenya Wajiunga na Wakenya kuadhimisha Miaka 36 ya Kifo cha Imam Khomeini Jijini Nairobi + Picha

Kikao hicho kilichobeba kauli mbiu: “Demokrasia ya Kidini kwa Mtazamo wa Imam Khomeini na Ayatollah Khamenei,” kiliwakutanisha Mabalozi, Wasomi, na Wananchi kujadili masuala ya Imani, Uongozi, na Utawala katika Muktadha wa Falsafa ya Kisiasa ya Kiislamu.

Wairan Wanaishi Nchini Kenya Wajiunga na Wakenya kuadhimisha Miaka 36 ya Kifo cha Imam Khomeini Jijini Nairobi + Picha

Balozi wa Iran nchini Kenya, Dkt. Ali Gholampour, aliongoza Kikao hicho na kutoa hotuba kuu iliyomuenzi Imam Khomeini (MA) kama Kiongozi wa Mapinduzi na Mwanafalsafa wa Kiroho mwenye ushawishi mkubwa hadi leo hii.

Wairan Wanaishi Nchini Kenya Wajiunga na Wakenya kuadhimisha Miaka 36 ya Kifo cha Imam Khomeini Jijini Nairobi + Picha

Miongoni mwa wazungumzaji mashuhuri waliokuwa katika Kikao hicho ni: Dkt. Ali Pormarjan, Mshauri wa Masuala ya Kitamaduni katika Ubalozi wa Iran Jijini Nairobi, na Balozi Esther Waringa, Rais wa Utawala wa Huduma za Umma, pamoja na wageni wengine mashuhuri.

Wairan Wanaishi Nchini Kenya Wajiunga na Wakenya kuadhimisha Miaka 36 ya Kifo cha Imam Khomeini Jijini Nairobi + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha