Tuzo hiyo imetolewa na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, kama ishara ya kutambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha misingi ya Utawala bora, Demokrasia, na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

1 Juni 2025 - 01:07

Kwa Mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii Tarehe 31 Mei, 2025 - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea Tuzo Maalum ya Heshima ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Spika Dkt. Tulia Amkabidhi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Tuzo Maalu ya Heshima Ya Bunge Jijini Dododma + Picha

Tuzo hiyo imetolewa na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, kama ishara ya kutambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha misingi ya Utawala bora, Demokrasia, na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Spika Tulia alisema kuwa Tuzo hiyo ni sehemu ya kuthamini juhudi za Rais Samia katika kuendeleza mahusiano mema kati ya mihimili ya dola na kuleta mageuzi yenye tija katika sekta mbalimbali nchini.

Spika Dkt. Tulia Amkabidhi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Tuzo Maalu ya Heshima Ya Bunge Jijini Dododma + Picha

Rais Samia amelishukuru Bunge kwa heshima hiyo kubwa na kuahidi kuendelea kushirikiana na Bunge katika kuwatumikia Watanzania kwa moyo wa uwajibikaji, mshikamano, na uadilifu.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Wabunge, pamoja na wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali.

Spika Dkt. Tulia Amkabidhi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Tuzo Maalu ya Heshima Ya Bunge Jijini Dododma + Picha

Spika Dkt. Tulia Amkabidhi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Tuzo Maalu ya Heshima Ya Bunge Jijini Dododma + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha