Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (a.s) -ABNA- Sherehe ya kufikia umri wa kubalehe na kutekeleza Hukumu za Kisheria (Taklif) kwa kundi la Wasichana imefanyika katika Mji Mkuu wa Senegal, Dakar, kwa juhudi za Jumuiya ya Wanawake ya Bibi Fatimah Zahra (s.a) chini ya Baraza la Wanazuoni wa Ahlul-Bayt nchini Senegal.

1 Juni 2025 - 23:43

Ayatollah Reza Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s), ambaye yuko nchini Senegal kwa mwaliko wa viongozi wa kidini wa nchi hiyo, alikuwa mgeni maalum katika hafla hiyo.

Habari Pichani | Sherehe ya Kufikia Umri wa Taklif kwa Wasichana wa Kisengali kwa Ushiriki wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s)

Sherehe hii ilikuwa ya heshima kubwa kwa wasichana waliofikia umri wa balehe, na ilijumuisha hotuba, mawaidha ya kidini, burudani ya kimaadili, na kuwapa zawadi wasichana waliofikia umri wa taklif (umri wa kuwajibika kidini kwa kuchunga na kutekeleza hukumu na sheria za kidini).

Habari Pichani | Sherehe ya Kufikia Umri wa Taklif kwa Wasichana wa Kisengali kwa Ushiriki wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s)

Your Comment

You are replying to: .
captcha