Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mitihani ya mwisho ya muhula wa kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2025 imeanza rasmi katika Chuo Kikuu cha Al-Mustafa (S) – Tawi la Dar es Salaam, Tanzania, chini ya mazingira ya kielimu na kiroho yanayojaa bidii na juhudi kubwa kutoka kwa Wanafunzi.
Chuo Kikuu cha Al-Mustafa (s), Dar-es-Salam, kinatilia mkazo mkubwa katika kuinua kiwango cha elimu kwa wanafunzi wake kupitia usimamizi wa karibu wa ratiba za masomo na upangaji makini wa mitihani katika vituo vyake vyote vya Sayansi ya Kidini. Masomo na mitihani ni sehemu muhimu ya safari ya kutafuta Sayansi ya kidini, kwani faida yake haijifungi tu kwenye tathmini ya nje ya uelewa wa Mwanafunzi, bali pia inakwenda mbali zaidi katika kuimarisha maadili, malezi na maendeleo ya kielimu na kiroho. Miongoni mwa manufaa hayo ni haya yafuatayo:
-
Kuthibitisha Maarifa na Kuimarisha Uelewa
Kuhudhuria masomo na kujitayarisha kwa mitihani kunasaidia katika kuhifadhi maarifa kichwani na kukuza uelewa wa kina wa mafundisho ya dini na akili. -
Kukuza Nidhamu na Umakini
Mitihani huwalea wanafunzi katika nidhamu, kuheshimu muda, na kuwapa hisia ya kuwajibika kwa elimu na ujumbe wa kidini. -
Kubaini Nguvu na Udhaifu
Mitihani ni fursa ya kutathmini maeneo ambayo Mwanafunzi ana nguvu nayo, pamoja na yale yanayohitaji juhudi zaidi na marejeo ya kina. -
Kuchochea Bidii na Kuendelea Kujifunza
Mitihani huwapa Wanafunzi motisha ya kuendelea na kujitahidi katika elimu, kwani huona matokeo ya juhudi zao na maendeleo waliyoyafikia. -
Kujiandaa kwa Majukumu ya Baadaye
Hatua hii ya kielimu inawaandaa wanafunzi kuchukua jukumu la kufundisha, kuhubiri, na kufanya utafiti wa kielimu kwa mujibu wa mahitaji ya wakati wa sasa. -
Kujilea Nafsi na Kujiimarisha Kimaadili
Katika mazingira ya Hawza, mitihani si tu kipimo cha maarifa, bali pia ni nafasi ya kujilea nafsi, kustahimili, na kujitakasa kwa ikhlasi katika kutafuta elimu, hali inayomjenga Mwanafunzi kimaadili na kumjaza ari ya juu.
Hakika elimu katika Hawza si mkusanyiko wa maalumati tu, bali ni ujenzi wa kina wa akili na roho, na Mitihani ni hatua mojawapo katika safari hii tukufu kuelekea ukamilifu wa kielimu na kibinadamu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape Wanafunzi wote Tawfiq na mafanikio katika mitihani yao, na awajaalie wawe miongoni mwa wabeba bendera ya elimu na dini, wanaoifanyia kazi kwa ajili ya Uislamu na jamii.
Your Comment