Shahada ya Imam (a.s) ni pigo kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu, hususan kwa wale wanaotambua nafasi yake tukufu na elimu yake adhimu.

3 Juni 2025 - 14:07

Burundi | Majlisi ya Maombolezo ya Shahadat ya Imam Muhammad Baqir (a.s) imefanyika katika Hawzat ya Imam Zainul Abidin (a.s) + Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kikao cha Maombolezo kwa ajili ya kuadhimisha Shahadat ya Imam Muhammad Baqir (as) kimefanyika katika Shule ya Imam Zainul Abidin (as) nchini Burundi, na kuhudhuriwa na walimu pamoja na wanafunzi.

Sheikh Sajjad Fawzi alitoa hotuba akieleza fadhila na daraja ya kielimu ya Imam Baqir (as), akibainisha kuwa alikuwa ni mtu Mcha Mungu na Mwenye Elimu kubwa katika zama zake, kama ambavyo vitabu vya kihistoria vinavyomtaja.

Alisisitiza kuwa shahada ya Imam (a.s) ni pigo kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu, hususan kwa wale wanaotambua nafasi yake tukufu na elimu yake adhimu.

Burundi | Majlisi ya Maombolezo ya Shahadat ya Imam Muhammad Baqir (a.s) imefanyika katika Hawzat ya Imam Zainul Abidin (a.s) + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha