Majlisi hiyo ilijumuisha usomaji wa Aya za Qur’an Tukufu, Hotuba za Maombolezo zilizozungumzia Historia ya Maisha ya Imam Baqir(as), pamoja na Mashairi ya Maombolezo yaliyodhihirisha huzuni kubwa ya tukio hilo.

4 Juni 2025 - 15:28

Hawza ya Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni, Dar-es-salaam - Imekuwa Kitovu cha Kumbukumbu ya Shahada ya Imam Muhammad Baqir (A.S) + Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Hawza ya Mabanati ya Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni, Dar-es-salaam, katika mazingira ya huzuni, masikitiko na unyenyekevu, imeadhimisha kumbukumbu ya Kuuliwa Shahidi kwa Imam Muhammad Baqir (A.S), Imam wa 5 katika mlolongo wa Maimam wa Ahlul-Bayt (A.S) kwa Mujibu wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ithna Asharia.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Walimu, Wanafunzi wa Hawza ya Bibi Zainab (SA), pamoja na Waumini wengi waliokusanyika kuadhimisha tukio hili tukufu na kupata mafunzo mbalimbali na mazuri yaliyopo katika maisha ya Imam Baqir (A.S) ambaye alijulikana zaidi kwa elimu, hekima na juhudi zake katika kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (A.S).

Hawza ya Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni, Dar-es-salaam - Imekuwa Kitovu cha Kumbukumbu ya Shahada ya Imam Muhammad Baqir (A.S) + Picha

Shughuli hiyo ilijumuisha usomaji wa aya za Qur’an Tukufu, hotuba za maombolezo zilizozungumzia historia ya maisha ya Imamu, pamoja na mashairi ya maombolezo yaliyodhihirisha huzuni kubwa ya tukio hilo.

Your Comment

You are replying to: .
captcha