Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin katika Khutba yake, alionyesha kuwa Imam Khomeini (RA) alikuwa mfano halisi wa Kiongozi aliyefanikisha Mapinduzi makubwa kwa msingi wa dini. Ujasiri wake, elimu yake, na utiifu kwa Allah vilimfanya awe nuru ya mabadiliko – si kwa Iran tu, bali kwa Ulimwengu mzima wa Kiislamu.

6 Juni 2025 - 22:16

Sala ya Ijuma | Khatibu - Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Maisha ya Imam Khomeini (RA) na Mchango wake katika kuikomboa Iran na Uislamu kwa ujumla"

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Sala ya Ijumaa leo hii imeswaliwa katika Chuo Kikuu cha Jamiat Al-Mustafa (s), Dar es Salaam Khatibu akiwa ni: Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin, ambapo katika Khutba yake ya  Sala ya Ijumaa aliangazia maisha ya Imam Khomeini (RA) na mchango wake katika kuikomboa Iran na Uislamu kwa ujumla. Ifuatayo ni sehemu ya Khutba ya Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin kuhusu maisha ya Imam Khomeini (RA), Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya Mwaka 1979,  na Mchango wake katika kuikomboa Iran na Uislamu kwa ujumla, na Mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Sala ya Ijuma | Khatibu - Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Maisha ya Imam Khomeini (RA) na Mchango wake katika kuikomboa Iran na Uislamu kwa ujumla"

1. Maisha ya Imam Khomeini (RA):

Imam Ruhullah Al-Musawi Al-Khomeini (RA) alizaliwa mwaka 1902 katika mji wa Khomein, Iran. Alikuwa Mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu, Fakihi, Mcha Mungu, na Kiongozi Mahiri wa Kisiasa. Alilelewa katika familia ya Wanazuoni na alipata elimu ya juu ya Fiqhi, Falsafa, na Ma'arifa katika Hawza ya Qum.

Katika maisha yake, Imam Khomeini (ra) alisimama kidete dhidi ya dhulma, udikteta, na ukandamizaji wa mabeberu, hasa Marekani na utawala wa kifalme wa Pahlavi uliokuwa umeegemea kwao kwa wakati huo. Alikataa kuishi chini ya utawala wa kimabavu usiozingatia mafundisho ya Uislamu na Sheria za Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Sala ya Ijuma | Khatibu - Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Maisha ya Imam Khomeini (RA) na Mchango wake katika kuikomboa Iran na Uislamu kwa ujumla"

2. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (1979):

Imam Khomeini (ra) aliongoza harakati za umma wa Iran zilizofikia kilele chake mwaka 1979 kwa kuuangusha utawala wa Shah Mohammad Reza Pahlavi. Mapinduzi haya hayakuwa tu ya kisiasa bali yalikuwa na msingi wa kidini na kifikra, yakihimiza:

  • a) Haki na usawa kwa raia wote.

  • b) Kujitegemea kisiasa na kiuchumi.

  • c) Kusimamisha mfumo wa kidini unaozingatia Fiqhi na maadili ya Kiislamu.

    Sala ya Ijuma | Khatibu - Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Maisha ya Imam Khomeini (RA) na Mchango wake katika kuikomboa Iran na Uislamu kwa ujumla"

3. Mchango Wake Katika Kuikomboa Iran na Uislamu

a) Kuikomboa Iran:

Imam Khomeini aliikomboa Iran kutoka mikononi mwa vibaraka wa kibeberu waliokuwa wakitawala kwa maslahi ya mataifa ya Magharibi. Alisimika mfumo mpya wa Wilayat al-Faqih, unaotambua uongozi wa mwanachuoni wa Kiislamu mwenye elimu, uadilifu, na uchungu kwa umma.

b) Kuleta Heshima kwa Uislamu:

Kwa mapinduzi haya, Imam Khomeini aliurudishia Uislamu heshima duniani. Aliweka bayana kuwa Uislamu si dini ya sala tu bali ni mfumo kamili wa maisha unaoweza kusimamia siasa, uchumi, elimu, na haki jamii.

c) Kuwasha Mwanga wa Harakati za Kiislamu Duniani:

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliwaamsha Waislamu duniani na kuwa chachu ya harakati za Kiislamu katika nchi mbalimbali. Ujumbe wake ulikuwa: “Simameni dhidi ya dhulma na tawala zisizo na haki, kwa jina la Mwenyezi Mungu na kwa kufuata mafundisho ya Qur’an na Ahlul-Bayt (as).”

Sala ya Ijuma | Khatibu - Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Maisha ya Imam Khomeini (RA) na Mchango wake katika kuikomboa Iran na Uislamu kwa ujumla"

4. Mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu:

  • 1- Kuanzishwa kwa mfumo wa kidini wenye uhuru wa kweli.

  • 2- Kujitegemea kisiasa na kijeshi.

  • 3- Kuendeleza utafiti wa kielimu, kiteknolojia na nyuklia kwa amani.

  • 4- Kuunga mkono harakati za ukombozi duniani, hasa Palestina.

  • 5- Kuonyesha kuwa Uislamu unaweza kuongoza Taifa kwa mafanikio.

Sala ya Ijuma | Khatibu - Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Maisha ya Imam Khomeini (RA) na Mchango wake katika kuikomboa Iran na Uislamu kwa ujumla"

Hitimisho:

Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin katika Khutba yake, alionyesha kuwa Imam Khomeini (RA) alikuwa mfano halisi wa Kiongozi aliyefanikisha Mapinduzi makubwa kwa msingi wa dini. Ujasiri wake, elimu yake, na utiifu kwa Allah vilimfanya awe nuru ya mabadiliko – si kwa Iran tu, bali kwa Ulimwengu mzima wa Kiislamu. Leo hii, wajibu wetu ni kuenzi fikra zake, kuendeleza mapinduzi haya kwa njia ya elimu, maadili, na muamala mwema.

Sala ya Ijuma | Khatibu - Samahat Sheikh Dkt. Reihan Yasin: "Maisha ya Imam Khomeini (RA) na Mchango wake katika kuikomboa Iran na Uislamu kwa ujumla"

Your Comment

You are replying to: .
captcha