Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sala tukufu ya Eid Al-Adh’ha ilisaliwa kwa taadhima kubwa katika Kituo cha Imam Reza (as) nchini Kenya siku ya Jumamosi, tarehe 7 Juni 2025, ambapo waumini wengi walihudhuria na kushiriki kwa unyenyekevu na kwa utulivu wa nyoyo katika ibada hiyo adhimu. Sheikh Jum'a Shughuli, akihutubia waumini baada ya Sala, aliwapongeza kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika ibada hiyo adhimu.

9 Juni 2025 - 23:39

Waumini Walijitokeza kwa Wingi Kusali Sala ya Eid Al-Adh'ha Katika Kituo cha Imam Reza (as), Kenya + Picha

Aidha, Sheikh Jum'a Shughuli alitoa salamu za Eid kwa waumini wote, na kuwaombea baraka katika siku hizi tukufu za Mwezi wa Dhul-Hijjah.Pia alimuomba Mwenyezi Mungu (swt) azikubali ibada na matendo ya kila mmoja, na amjaalie kila Muislamu kudumu katika utiifu wa kweli kwa Mola wake Mtukufu.

Waumini Walijitokeza kwa Wingi Kusali Sala ya Eid Al-Adh'ha Katika Kituo cha Imam Reza (as), Kenya + Picha

Hafla hiyo iliambatana na hali ya mshikamano, upendo na ari ya kiroho iliyoakisi utukufu wa siku hiyo katika maisha ya Waislamu.

Waumini Walijitokeza kwa Wingi Kusali Sala ya Eid Al-Adh'ha Katika Kituo cha Imam Reza (as), Kenya + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha