Katika sehemu ya sherehe, mmoja wa wanafunzi wa muhula wa tano alitoa hotuba juu ya umuhimu wa kujifunza na kufundisha suala la Wilayat (Kufuata uongozi wa kiroho wa Amirul-Muuini Ali bin Abi Tali na Ahlul-Bayt amani iwe juu yao).

14 Juni 2025 - 22:36

Sherehe ya Eid ya Ghadir - Hawza ya Hazrat Zainab (sa) Kigamboni - Dar-es-Salaam, Tanzania + Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Kwa mnasaba wa Eid Tukufu ya Ghadir, sherehe maalum iliyoandaliwa siku ya Jumamosi tarehe 14 Juni, 2025 imefanyika katika Ukumbi wa Hawza ya wasichana ya Hazrat Zainab (sa) iliyopo Kigamboni - Dar-es-Salaam, Tanzania. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na wanafunzi wote wa chuo hiki cha Mabinti na ilidumu kwa muda wa nusu saa.

Sherehe ya Eid ya Ghadir - Hawza ya Hazrat Zainab (sa) Kigamboni - Dar-es-Salaam, Tanzania + Picha

Katika sehemu ya sherehe, mmoja wa wanafunzi wa muhula wa tano alitoa hotuba juu ya umuhimu wa kujifunza na kufundisha suala la Wilayat (Kufuata uongozi wa kiroho wa Amirul-Muuini Ali bin Abi Tali na Ahlul-Bayt amani iwe juu yao). Aidha, alisisitiza kuwa katika kipindi hiki cha sasa, umoja na mshikamano ni jambo la msingi, na hilo haliwezi kupatikana isipokuwa kwa kueneza utamaduni wa Wilayat. Aliwahimiza wanafunzi kuchunguza kwa makini tukio la Ghadir ili waweze kuufikisha ujumbe wake kwa jamii kwa njia iliyo bora zaidi.

Sherehe ilianza kwa kisomo cha Qur’an Tukufu kilichoendeshwa na mmoja wa wanafunzi wa muhula wa sita, na hatimaye kukamilika kwa usomaji wa Qaswida na Utenzi.

Your Comment

You are replying to: .
captcha