Watu wengi wajitokeza katika Mji wa Qom kuaga miili mitukufu ya Mashahidi sita - Viongozi wa Kijeshi
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Waumini wengi wamejitokeza Leo hii katika Sala ya Ijumaa iliyossliwa katika Mji wa Qom Iran iliyoitwa nchi nzima kuwa ni Ijumaa ya Ghadhabu na Ushindi. Baada ya Sala ya Ijumaa walishiriki katika Maandamano dhidi ya Utawala Haram wa kizayuni sambamba na zoezi muhimu la kuaga Miili Mitukufu ya Mashahidi sita - Viongozi wa Kijeshi waliouliwa katika shambulizi la uchokozi la Israel lililoibua Mwanzo wa vita inayoendelea hivi sasa.
Ikumbukwe kuwa baada ya shambulizi hilo la uchokozi la Israel dhidi ya ardhi ya Iran, Iran ilianza Rasmi Operesheni yake Kali ya Kijeshi inayoitwa: "Ahadi ya Kweli 3" dhidi ya Utawala huu haram ndani ya Mashariki ya Kati unaoendelea kuikalia kimabavu na kidhulma nchi ya Palestina.
Your Comment