Mada hii kwa hakika ni yenye umuhimu mkubwa kwani inawasaidia Waislamu kufahamu jinsi ya kuishi kwa kuzingatia mafunzo ya A'shura, kama vile: Ustahamilivu, kuinusuru haki, na kupigania ukweli na uadilifu hata kama ni kwa gharama ya kuyatoa muhanga maisha yako kwa ajili ya Uislamu.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ijumaa ya kwanza ya mwaka mpya wa Kiislamu ( Muharram - 1447 Hijria) imeswaliwa ikiambatana na uhuishaji wa Majalis za Muharram, ikiwa ni ishara nzuri ya kuanza mwaka mpya wa Hijria kwa njia ya kukumbusha na kuhuisha masuala muhimu ya Kihistoria na Kidini.
Sala hii ya Ijumaa leo hii imeongozwa na Hojjatul Islam wal-Muslimin, Sheikh Abdul Majid Nasser katika Masjid ya Jamiat al-Mustafa (s), Dar es Salaam, Tanzania, ambapo katika Khutba yake amezungumzia mada muhimu yenye maudhui hii:
"Jinsi ya kuishi katika Mwezi wa Muharram kulingana na matukio muhimu ya Mwezi huu".
Mwezi wa Muharram ni Mwezi Mtukufu na wa kihistoria kwa Waislamu, hasa kwa tukio la Karbala ambalo linahusisha ujasiri na dhabihu ya Imam Hussein (A.S) na wafuasi wake waliouliwa Kishahidi pamoja naye katika Ardhi ya Karbala.
Mada hii kwa hakika ni yenye umuhimu mkubwa kwani inawasaidia Waislamu kufahamu jinsi ya kuishi kwa kuzingatia mafunzo ya A'shura, kama vile:
Ustahamilivu, kuinusuru haki, na kupigania ukweli na uadilifu hata kama ni kwa gharama ya kuyatoa muhanga maisha yako kwa ajili ya Uislamu.
Athari ya Kuishi Kwa Kulingana na Matukio ya Muharram
1. Kujitolea na Haki: Kupitia mifano ya Imam Hussein (A.S), Waislamu wanahamasishwa kuishi kwa njia inayoheshimu haki, kupigania ukweli na kupinga uovu popote pale ulipo.
2. Maadili ya Mwezi wa Muharram: Huu ni mwezi wa madhumuni, tofauti na tafakuri. Waislamu wanahimizwa kutafakari juu ya mapenzi ya Allah, imani yao, na maadili ambayo yametumika katika vita ya Karbala.
3. Kufundisha Vijana: Programu kama hizi ni nafasi nzuri ya kuelimisha vijana kuhusu umuhimu wa upendo wa Imam Hussein (A.S.) na jinsi ya kuchukua mafunzo kutoka kwa tukio la Karbala na kuyaingiza kwenye maisha ya kila siku.
Athari ya Majalis za Muharram kwa Waislamu wa Tanzania
Kwa Waislamu wa Tanzania, hasa katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Dodoma, Arusha n.k, kushiriki katika programu kama hizi kunawawezesha Waislamu kudumisha urithi wa kidini na kutoa nafasi kwa jamii kuungana katika Majalis za Kidini.
Kwa vijana, ni fursa ya kujenga uhusiano wa karibu na urithi wa kihistoria wa Uislamu na kuimarisha mshikamano wa kidini.
Your Comment