Majalis / Vikao hivi vitaendelea kutoa fursa ya kutafakari kuhusu ujumbe wa A'shura kwa Wanafunzi na jamii ya kielimu bali Umma mzima wa Kiislamu wenye kiu kubwa ya kujua ukweli na uhakika, na kufuata Haki na Uadilifu.

28 Juni 2025 - 21:07

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii Tarehe (28 - 06- 2025), Majalis (Vikao) vya Kuadhimisha Shahada ya Imam Hussein (AS) vimeendelea kwa hamasa kubwa katika Chuo Cha Jamiat Al-Mustafa   - Dar-es-salaam - Tanzania - na Khatibu wetu kwa Leo hii alikuwa ni: Hojjat al-Islam wal-Muslimin, Samahat Sheikh Abdul Majid Nasser.

Majalis (Vikao) vya Kuadhimisha Shahada ya Imam Hussein (AS) katika Chuo Cha Jamiat Al-Mustafa   - Dar-es-salaam - Tanzania + Picha

Somo / Mada ya leo ilihusiana na: "Kuingia kwa Imam Hussein (A.S) katika Karbala"

Kuhusu mada hii, Sheikh afafanua kwa kirefu zaidi akibainisha ilikuwaje Imam Hussein (as) akafika katika Ardhi ya Karbala, na baada ya kufika hali na mazingira yalikuwa vipi?, Je, alitoka Madina akisudia kwenda katika Ardhi ya Karbala?.n.k yote hayo yamewekwa bayana kupitia ubainishaji Maridhawa wa Khatibu wa Majalis hii.

Mikutano na Vikao mbalimbali vya kuendeleza kuadhimisha Shahada ya Imam Hussein (AS) vinaendelea kufanyika katika Chuo hiki Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa(s) kwa kila Siku, ambapo Matukio mbalimbali ya kihistoria yaliyojaa mafunzo mbalimbali kwa Umma wa Kiislamu yanaendelea kuchambuliwa na wahadhiri mbalimbali kupitia mimbari ya Haki ya Imam Hussein (as).

Majalis (Vikao) vya Kuadhimisha Shahada ya Imam Hussein (AS) katika Chuo Cha Jamiat Al-Mustafa   - Dar-es-salaam - Tanzania + Picha

Katika Vikao hivi, yanaelezwa mengi yenye faida kemkem kuhusiana na umuhimu wa mapambano ya Imam Hussein (AS) kwa ajili ya Haki na Mabadiliko. 

Qur'an inasema: "Mwenyezi Mungu habadilishi yaliyopo kwa watu mpaka watu wenyewe waamue kufanya Mabadiliko".

Hiki ndicho alichokifanya Imam Hussein (as) ambapo alisimama kwa Msimamo Madhubuti na akaamua kuitetea Dini ya Haki na kuhuisha mafunzo yake ya Haki, na kuleta Mabadiliko chanya katika Umma wa Kiislamu. 

Leo hii Umma unajivunia matokeo chanya ya Mapinduzi ya Imam Hussein (as) yaliyoanzia katika Ardhi ya Karbala.

Majalis kama hizi ni fursa adhimu ya kueneza maarifa ya A'shura na kufafanua malengo ya Haki ya Imam Hussein (AS) kwa Waislamu ili wajue ukweli na uhakika uliopo katika Mapinduzi ya Imam Hussein (as).

Majalis (Vikao) vya Kuadhimisha Shahada ya Imam Hussein (AS) katika Chuo Cha Jamiat Al-Mustafa   - Dar-es-salaam - Tanzania + Picha

Tanbihi:

Vikao hivi vitaendelea kutoa fursa ya kutafakari kuhusu ujumbe wa A'shura kwa Wanafunzi na jamii ya kielimu bali Umma mzima wa Kiislamu wenye kiu kubwa ya kujua ukweli na uhakika, na kufuata Haki na Uadilifu.

Majalis (Vikao) vya Kuadhimisha Shahada ya Imam Hussein (AS) katika Chuo Cha Jamiat Al-Mustafa   - Dar-es-salaam - Tanzania + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha