Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Majlisi ya Imam Hussein (as) imefanyika katika kituo cha Bilal Muslim Mission of Tanzania - Moshi Mjini. Waumini mbalimbali wanajitokeza kwa wingi kila siku kushiriki katika Majalis za Aba Abdillah Al-Hussein zinazofanyika katika vituo mbalimbali vya Bilal Muslim Mission of Tanzania. Ujumbe wa Imam Hussein (as) na Mapinduzi yake ya Karbala vinazidi kueleweka zaidi kwa umma wa kiislamu na kuhuishwa zaidi kila mwaka na sasa waumini wengi wanaijua na kuendelea kuijua misheni ya Imam Hussein (as) na Falsafa yake.
1 Julai 2025 - 17:16
News ID: 1703507
Your Comment