Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Majlis mbalimbali zinaendelea katika Husseiniyya Jijini Arusha katika kuomboleza na kutoa masomo mbalimbali juu ya malengo ya harakati ya kimapinduzi ya Imam Hussein (as) aliyoifanya katika Ardhi ya Karbala, Mapinduzi ambayo hadi leo hii yanaendelea kutoa matunda yake mazuri kwa walimwengu wote, hususan kwa ulimwengu wa Kiislamu. Waumini mbalimbali wanajitokea katika Majalis hizi kwa ajili ya kujifunza masomo mbalimbali yaliyomo katika Mapinduzi ya Karbala yaliyoongozwa na Imam Hussein (as), Mjukuu Kipenzi wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w).
1 Julai 2025 - 18:34
News ID: 1703869
Your Comment