Kupandishwa kwa Bendera hiyo ni ishara ya msimamo wa milele wa haki dhidi ya dhulma, na ni mwaliko kwa Waumini kujiandaa kuhudhuria katika Majalisi, kushiriki katika kuandaa Mashairi, na khutba mbalimbali zinazobainisha ujumbe wa Karbala na mafundisho ya Imam Husein (a.s).
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Moja ya matukio muhimu katika ratiba za Mwezi wa Muharram katika Masjidul Ghadir ni hafla ya kupandisha Bendera ya Imam Hussein (as) - Juu kabisa ya Masjid al-Ghadir, ambapo inachukuliwa kuwa alama rasmi ya kuanza kwa Mwezi wa Mtukufu wa Muharam na Majlisi za Maombolezo ya A'shura.
Aidha, tukio hili linaashiria kuingia kwa kipindi cha huzuni kwa Waislamu, hususan Wapenzi na wafuasi wa Ahlulbayt (a.s), ambapo wanaomboleza tukio la kuhuzunisha na la kihistoria la kuuawa kwa kinyama kwa mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Husein (a.s), pamoja na masahaba wake waaminifu katika ardhi ya Karbala.

Your Comment