Samahat Sheikh aliwahimiza Waumini kuwa makini na waangalifu, kuwa wenye hekima, na waadilifu, wakijilinda dhidi ya athari za tamaduni na mitazamo ya kimagharibi inayopingana na misingi ya Kiislamu. Lengo ni kuilinda jamii kwa msingi wa Maarifa, Taq'wa, na ufuasi wa kweli wa Ahlul-Bayt (a.s).
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo Siku ya: Ijumaa, Tarehe: 8 Muharram 1447 H inayosadifiana na Tarehe 4 Julai, 2025, Sala ya Ijumaa imeswaliwa katika Madrasa ya Wasichana wa Kiislamu ya Hazrat Zainab (sa), iliyopo Kigamboni Jijini Dar-es-salaam - Tanzania.
Khatibu wa Sala hii: Hujjatul Islam wal Muslimin Sheikh Dkt. Saleh Maulid.
Katika Khutba yake, Sheikh Dkt. Saleh aligusia mambo mawili muhimu katika sehemu ya Kwanza na ya Pili ya Khutba ya Ijumaa:
1_Sehemu ya Kwanza: Taq'wa (Kumcha Mwenyezi Mungu)
Samahat Sheikh alisisitiza kuwa: “Kila mtu anayetaka kukamilika kimaadili na kiroho, lazima awe na msingi wa Taq'wa. Bila Taq'wa, mtu anakumbwa na matatizo mbalimbali katika nyanja zote za maisha.
Hivyo ni lazima tujitahidi kujiandaa sisi na familia zetu kwa Taq'wa ili tuwe karibu na Ahlul-Bayt (a.s).”
2_Sehemu ya Pili: Jihadi ya Kidijitali (Jangwa la Vita vya Kisaikolojia / Vita Baridi)
Katika sehemu ya pili, Sheikh letu alizungumzia kuhusu changamoto ya sasa ya vita laini au baridi (janga la vita vya kimtazamo na kifikra), na akasema:
“Maisha ya sasa yamekumbwa na vita laini (baridi), ambavyo mara nyingi hatuvitambui kwa utambuzi wa haraka haraka.
Mambo kama vile kuvaa, kula, namna ya kuzungumza na watu, na hata mabishano yasiyo na maana - haya yote ni sehemu ya vita laini. Watu wengi wanaathiriwa bila kujua na vita hii.”
Mwisho wa Khutba yake:
Samahat Sheikh aliwahimiza Waumini kuwa makini na waangalifu, kuwa wenye hekima, na waadilifu, wakijilinda dhidi ya athari za tamaduni na mitazamo ya kimagharibi inayopingana na misingi ya Kiislamu.
Lengo ni kuilinda jamii kwa msingi wa Maarifa, Taq'wa, na ufuasi wa kweli wa Ahlul-Bayt (a.s).
Your Comment