Majlis hii iliambatana na Mashairi ya Maombolezo, Masimulizi ya historia ya Karbala, na ujumbe wa kusimama imara kwa ajili ya Haki, kama wanavyotufundisha Ahlul-Bayt (a.s) wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo, Alhamisi, 4 Julai 2025, Maombolezo kwa ajili ya kuadhimisha Shahada ya Imam Hussein (a.s) yamefanyika katika Taasisi ya Kimataifa ya Al-Mustafa (s), Dar es Salaam, Tanzania.
Mzungumzaji akiwa: Sheikh Suleiman. Mada: Ali Akbar (as).
Katika mawaidha haya, Sheikh Suleiman alieleza kuhusu nafasi tukufu ya Ali Akbar (a.s) - kijana wa Imam Hussein (a.s) - aliyekuwa Mcha Mungu, Jasiri, na Mwenye kufanana zaidi na Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa Maumbile, Mazungumzo na tabia njema.
Majlis hii iliambatana na Mashairi ya Maombolezo, Masimulizi ya historia ya Karbala, na ujumbe wa kusimama imara kwa ajili ya Haki, kama wanavyotufundisha Ahlul-Bayt (as) wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Waumini na Wanafunzi walihudhuria kwa wingi wakionyesha mapenzi yao makubwa kwa Imam Hussein (a.s) na Kizazi Kitukufu cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Your Comment