Majlisi hii ilifanyika kwa hali ya utulivu, huzuni na mapenzi makubwa kwa Imam Hussein (a.s), ikiwa ni njia ya kudumisha ujumbe wa Karbala na kushikamana na njia ya haki.

4 Julai 2025 - 22:37

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, tarehe 8 Muharram 1447 H / 4 Julai 2025, Wanafunzi wa Madrasa ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa) – Kigamboni – Dar-es-Salaam, Wameendelea kumuenzi Imam Hussein (a.s) kwa Maombolezo ya Muharram.

Majlisi ya Muharram: Wanafunzi wa Madrasa ya Hazrat Zainab (sa), Waonyesha Mapenzi Makubwa kwa Ahlul-Bayt (a.s) katika Maombolezo ya Muharram + Picha

Majlisi ya Muharram: Wanafunzi wa Madrasa ya Hazrat Zainab (sa), Waonyesha Mapenzi Makubwa kwa Ahlul-Bayt (a.s) katika Maombolezo ya Muharram + Picha

Majlisi hii ya Maombolezo ya Imam Hussein (a.s) imefanyika leo hii Siku ya Ijumaa kupitia juhudi za Madrasa hii ya Wasichana kwa jina: Madrasa Hazrat Zainab (sa), ambapo katika ukumbi wa Madrasa wa Zainabiyya.

Majlisi ya Muharram: Wanafunzi wa Madrasa ya Hazrat Zainab (sa), Waonyesha Mapenzi Makubwa kwa Ahlul-Bayt (a.s) katika Maombolezo ya Muharram + Picha

Majlisi hii tukufu limehudhuriwa kwa wingi na Wanafunzi wenye mapenzi makubwa kwa Ahlul-Bayt (a.s), na imefanyika kwa kujumuisha vipengele mbalimbali vya kiroho kama ifuatavyo:

  1. Kusoma Qur'an Tukufu: Kisomo hichi cha Qur’an Tukufu kwa ajili ya ufunguzi wa Majlisi, kimesomwa na Mwanafunzi:Fatma Mawga.
  2. Ziyarat A’shura: Ilisomwa na Mwanafunzi: Amina Muni Jum’a.
  3. Khutba: Iliwasilishwa na Mwanafunzi: Rahmat Abdin, kuhusu “Mafunzo Kutoka A’shura”.
  4. Mashairi ya Kidini: Yalisomwa na Mwanafunzi: Mwana Mko.
  5. Maombolezo na Matam (sina): Yalifanyika kwa pamoja na wanafunzi wote.
  6. Kusoma Du'a Samat: Ilisomwa kwa pamoja na wanafunzi wote.
  7. Swala ya Jamaa ya Magharibi na Isha: Iliswaliwa kama hitimisho la Majlisi.

    Majlisi ya Muharram: Wanafunzi wa Madrasa ya Hazrat Zainab (sa), Waonyesha Mapenzi Makubwa kwa Ahlul-Bayt (a.s) katika Maombolezo ya Muharram + Picha

Majlisi hii ilifanyika kwa hali ya utulivu, huzuni na mapenzi makubwa kwa Imam Hussein (a.s), ikiwa ni njia ya kudumisha ujumbe wa Karbala na kushikamana na njia ya haki.

Your Comment

You are replying to: .
captcha