Kila mtu atafufuliwa na kile anachokipenda, hata kama mtu atapenda jiwe na kulifanya kuwa ndio kiongozi wake, basi atafufuliwa pamoja na jiwe hilo. Wafuasi wa Muovu Yazid bin Muawia na Bani Umaiyya, Mwenyezi Mungu awafufue pamoja na muovu huyo na Kizazi hicho cha Bani Umaiyya, na Wafuasi na wapenzi wote wa Imam Hussein (as) na Ahlul-Bayt (as), awafufue pamoja na Imam Hussein (as) na Kizazi Kitukufu cha Ahlul-Bayt (as) kwa ujumla.
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mwenyezi Mungu atulipe sisi na nyinyi malipo mema na makubwa kwa msiba wa Aba Abdillah Al-Hussein(as). Imamu Hussein (a.s) amesema:
/ «من لحق بي استشهد، ومن لم يلحق بي لم يُدرك الفتح» “Atakayeungana nami basi atakuwa Shahidi, na asiyeungana nami hatofikia ushindi.”
Kauli hii (“Atakayeungana nami basi atakuwa Shahidi, na asiyeungana nami hatofikia ushindi”), ina maana kwamba yeyote atakayejiunga (au kuambatana au kuandamana) nami atauawa Kishahidi, na yeyote ambaye hatajiunga (hataandamana au kuambatana) nami hatapata nusra na ushindi. Sentensi hii inatokana na maneno ya Imam Hussein (AS) na inabainisha ukweli kwamba kuungana na Imam Hussein (AS) katika Mapinduzi ya Karbala kunamaanisha kuuawa Shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu na katika kutetea Uislamu na Haki (na hapa shaka kuwa: Kuuawa kishahidi kwa ajili ya kutetea ukweli, haki na Uislamu ni Furaha (Saada) kubwa, na ni baraka na heshima), ama wale ambao hawatajiunga (hawataungana) naye (na kuwa pamoja naye) katika njia hii, hao watanyimwa furaha ya nusra na ushindi wa kweli na halisi.
Alhamdulillah, kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita, mwaka huu pia Taasisi ya Kiislamu ya "Hujjatul Asr (a.t.f.s) of Tanzania", inaendelea na Majlisi za kila siku za Maombolezo ya Bwana wa Mashahidi, Aba Abdillah Hussein bin Ali (a.s) katika Mwezi huu Mtukufu wa Muharram.
Na leo hii, Siku ya Nane ya Mwezi wa Muharram 1447 H, umeshuhudiwa mwendelezo wa Majlisi hizo za Maombolezo ya Imam Hussein (as) katika Jiji la Dar es Salaam, Tanzania, iliyoratibiwa na Taasisi hii ya Kiislamu ya "Hujjatul Asr Society Of Tanzania" chini ya Usimamizi na Uongozi wa: Samahat Al-Sayyid Arif Ali Naqvi.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu atukubalie matendo mema, atuthibitishe katika njia ya Imam Hussein (a.s), na atufufue kesho siku ya Kiyama tukiwa pamoja naye na Ahlul-Bayt (as) kwa ujumle tunaowapenda na kuwafuata, kama riwaya inavyosema kuwa: Kila mtu atafufuliwa na kile anachokipenda, hata kama mtu atapenda jiwe na kulifanya kuwa ndio kiongozi wake, basi atafufuliwa pamoja na jiwe hilo. Wafuasi wa Muovu Yazid bin Muawia na Bani Umaiyya, Mwenyezi Mungu awafufue pamoja na muovu huyo na Kizazi hicho cha Bani Umaiyya, na Wafuasi na wapenzi wote wa Imam Hussein (as) na Ahlul-Bayt (as), awafufue pa moja na Imam Hussein (as) na Kizazi Kitukufu cha Ahlul-Bayt (as) kwa ujumla.
Your Comment